Kwa upana zaidi, Elimu ni tendo au uzoefu wenye athari ya
kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika
dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa kimaksudi na jamii
kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi
kingine.
Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, hesabu, sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu. Kuna elimu maalum kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wale wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbusho, maktaba pamoja na mtandao na tajriba za maisha.
Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya kimsimgi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya Maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, kijamii na utamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.
Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka wa 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya kiteknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.
Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na wakfu zina historia ndefu zaidi.
Masomo ya viwango vya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza.[[]] kufuzu. Idadi kubwa ya watu katika nchi zinazoendelea (hadi kufikia asilimia 50%) wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. kwa hivyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyikazi walioelimika.[onesha uthibitisho]
Elimu badala mara nyingi huwa ni matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya kijadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na maswala fulani ya elimu hiyo ya kijadi.[onesha uthibitisho] Elimu badala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule za badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa kivyao, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu vilevile husababisha hali ya umoja.[onesha uthibitisho] .
Kuingizwa kwa mbinu za asili kama vile kujua, kusoma, kuelekeza, kufunza na kusoma kama njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanafunzi/wanagenzi na walimu/waelekezi wanaweza kufaidika kutokana na elimu kwa njia ya kiasili iliyokuza, kutumia na kuendeleaza uhamasishaji wa tamaduni za kiasili.[2]
Kwa wanafunzi au wagenzi na walimu au waelekezi, kuwekwa pamoja kwa mbinu hizi mara nyingi huongeza fanaka, matarajio na matokeo ya elimu. Hili huafikiwa kwa kutoa elimu inayooana na taswira zao za asili, mazoea na mitiazamo yao ya ulimwengu. Kwa wanafunzi na walimu wasio wa asili, elimu ya aina hii ina athari ya kuongeza ufahamu wa tamaduni zao za kibinafsi na mazoea ya jumla ya umma na watu wanaowazunguka, hivyo basi kukuza heshima na kuthamini tamaduni za wanajamii hizo.
Katika elimu na mafunzo, kujumuishwa kwa maarifa ya kiasili, tamaduni, maono, mitazamo na dhana katika mitaala, vifaa vya kuelekeza na vitabu vya kozi vina athari kubwa kama ile ya kujumuisha mbinu za asili katika elimu ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Walimu na wanafunzi wa kisasa wana heshima, hamasa na maridhio kwa jamii na watu wa kienyeji kutokana na elimu husishi wanayopata.[3]
Mfano mkuu unaoonyesha mbinu na maudhui ya asili yanaweza kukuza matokeo yaliyotajwa hapo juu undhihirika katika elimu ya juu nchini Kanada. Kwa sababu ya sheria fulani, dhamira ya kuongeza mafanikio kwa wanafunzi wa elimu asili na kukuza maadili ya jamii ya kitamanduni, kuingizwa kwa mbinu na maudhui ya asili katika elimu huonwa kuwa jukumu na wajibu wa serikali na taasisi za elimu zenye mamlaka.[4]
Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo[11] ya kujifunza ndiyo ya kawaida:[12]
Teknolojia za habari na mawasiliano (ICT) ni "seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda, kueneza na kuongoza habari."[17] Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao, teknolojia za kusambaza habari (redio na televisheni) na simu. Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao zinavyoweza kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi.[18] Teknolojia za habari na mawasiliano za awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.[19]
Matumizi ya tarakilishi na mtandao bado ni changa (ikiwa vinatumika) katika nchi zinazoendelea, na hii ni kwa sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa hutumiwa kwa pamoja bali siyo mbinu moja pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za elimu katika kijiji fulani kule Sri Lanka.[20] Chuo kikuu cha Uingereza (UKOU) kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa chapa na kuongezea redio, runinga na hivi majuzi programu zilizounganishwa na kompyuta.[21] Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha Indira Gandhi nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa, video, redio, televisheni na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.[22]
Dhana ya “masomo yanayosaidiwa kwa Kompyuta” (CAL) limetumiwa kwa wingi kuelezea teknolojia katika masomo.
Katika kiwango cha mtu binafsi, kuna maandishi yenye uhusiano na kazi ya Jacob Mincer, [27] ya jinsi mapato yanahusiana na elimu na rasilimali ya mtu binafsi. Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa unazunguka jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.[28]
Wataalam wa uchumi Samwel Bowels na Herbert Ginits walitoa maoni kwamba kulikuwa na ubishi asili katika elimu nchini Marekani kati ya shabaha ya kidemokrasia shirikishi yenye usawa na faida ya mapato ya kikapitolisti yaliyodokeza hali ya kutokuwa na usawa.[29]
Siku hizi aina fulani ya elimu ni jambo la lazima kwa watu wote katika nchi nyingi. Kwa sababu ya ongozeko la watu na kuenea kwa elimu ya lazima, Shirika La Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepiga hesabu ya kwamba miaka 30 ijayo, watu wengi zaidi watapata elimu rasmi katika historia ya binadamu ulimwenguni.[30]
Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na bayolojia.[onesha uthibitisho] . Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo.[onesha uthibitisho] Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalum, sayansi tambuzi na sayansi masomo.[onesha uthibitisho] Katika vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia vimehifadhiwa katika vitivo vya elimu. Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.
Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko faida za elimu ya muda mrefu.[onesha uthibitisho] Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto wao shuleni.[onesha uthibitisho] Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao kurudishwa shuleni.[onesha uthibitisho]
Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na idadi kubwa ya watu.[onesha uthibitisho] Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.
Barani Afrika, shirika la NEPAD limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi. Vikundi vya kibinafsi kama vile The Church Of Jesus Christ Of Latter Days Saints, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kutokana na usaidizi wa raisi wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.
Elimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume[onesha uthibitisho], haswa kwa watoto wachanga. Kinyume na dhana ya kawaida[onesha uthibitisho], kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, kidini au ya dunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya maisha ya utu uzima.[34]
Walimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya wanafunzi wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, hesabu, sayansi na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani, kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu. Kuna elimu maalum kwa wale wanaohitaji ujuzi wa kitaaluma, kama vile wale wanaohitaji kuwa marubani. Juu ya hayo, kuna nafasi nyingi za elimu katika viwango vingine visivyo rasmi kama vile majumba ya ukumbusho, maktaba pamoja na mtandao na tajriba za maisha.
Haki ya kusoma imeweza kuelezwa kuwa haki ya kimsimgi ya binadamu katika kifungu cha pili cha itifaki ya kwanza ya Maagano ya haki za binadamu barani Ulaya kuanzia mwaka wa 1952 ambapo wanachama wote wanashurutishwa kuhakikisha elimu kwa wote. Katika kiwango cha kimataifa, Mapatano ya Umoja wa Mataifa ya haki za kiuchumi, kijamii na utamaduni katika mwaka wa 1966 yanahakikisha haki hii katika kifungu cha 13.
Yaliyomo
Mifumo ya elimu rasmi
Elimu ni dhana inayorejelea namna ambayo wanafunzi wanaweza kujifunza kitu:- Mwongozo unarejelea urahisishaji wa somo na hulenga kutambua shabaha zilizobuniwa na mwalimu au mbinu zingine za kufunza.
- Kufunza kunarejelea matendo halisi ya mwalimu yanayonuia kupasha elimu kwa wanafunzi.
- Kujifunza hurejelea masomo yenye mtazamo unaolenga kuwapa wanafunzi elimu, ujuzi na uwezo unaoweza kutumika punde tu wakamilishapo kipindi cha masomo.
Elimu Ya Msingi
- Masomo ya msingi huchukua kati ya miaka 5-7 ya kwanza ya elimu rasmi. Kwa jumla elimu ya juu hujumulisha miaka 6-8 ya masomo kuanzia mwaka wa tano au sita, lakini hutofautiana baina na kati ya nchi. Asilimia 70 ya watoto waliotimu umri wa kujiunga na shule hujiandikisha katika masomo ya msingi kote ulimwenguni na viwango hivi vinaongezeka.[1] Chini ya Elimu kwa mipango yote inaendeshwa na UNESCO, nchi nyingi wana nia ya kufanikisha zima uandikishaji katika elimu ya msingi ifikapo mwaka 2015, na katika nchi nyingi, ni lazima kwa watoto kupata elimu ya msingi.Chini ya mpango wa elimu kwa wote ulioanzishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja Wa Mataifa (UNESCO), nchi nyingi zimejitole
Elimu Ya Shule za Upili
Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka wa 1910 na ilisababishwa na kuwepo kwa biashara kubwa na maendeleo ya kiteknolojia viwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa na mtaala uliolenga maarifa ya kazi za ofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwa mwajiri kwani uimarishaji wa huduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushusha gharama kwa waajiri huku waajiriwa wakinufaika na mishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.
Barani Ulaya, shule za sarufi au akademia zilikuwepo hata katika miaka ya 1500. Shule za umma au zile za kulipa karo au hata shule za ufadhili na wakfu zina historia ndefu zaidi.
Elimu ya juu
Masomo ya viwango vya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza.[[]] kufuzu. Idadi kubwa ya watu katika nchi zinazoendelea (hadi kufikia asilimia 50%) wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. kwa hivyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyikazi walioelimika.[onesha uthibitisho]
Elimu Ya Ngumbaru
Elimu Badala
Elimu badala mara nyingi huwa ni matokeo ya mabadiliko katika elimu yaliyotokea katika misingi mbalimbali ya falsafa ambayo kwa kawaida ni tofauti na elimu ya kijadi ya lazima. Mabadiliko mengine yana misingi ya kisasa, kiutafiti au kifalsafa, ilhali mengine ni miungano isiyo rasmi kati ya walimu na wanafunzi wasioridhika na maswala fulani ya elimu hiyo ya kijadi.[onesha uthibitisho] Elimu badala hii ambayo ni pamoja na shule za tabia, shule za badala, shule zinazojitegemea na masomo ya nyumbani hutofautiana pakubwa kivyao, lakini zote hutilia maanani umuhimu wa idadi ndogo ya wanafunzi darasani na mahusiano ya karibu kati ya wanafunzi na walimu vilevile husababisha hali ya umoja.[onesha uthibitisho] .
Elimu ya asili
Kuongezwa kwa ruwaza za elimu ya asili (mbinu na maudhui yake) ndani ya elimu badala katika eneo la mfumo wa elimu rasmi na elimu isiyo rasmi kumewakilisha kipengele muhimu kilichochangia ufanisi wa mfumo wa elimu asili kwa wanajamii asili walioamua kufuata njia hii; hii ikiwa ni pamoja na wanafunzi na walimu.Kuingizwa kwa mbinu za asili kama vile kujua, kusoma, kuelekeza, kufunza na kusoma kama njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wanafunzi/wanagenzi na walimu/waelekezi wanaweza kufaidika kutokana na elimu kwa njia ya kiasili iliyokuza, kutumia na kuendeleaza uhamasishaji wa tamaduni za kiasili.[2]
Kwa wanafunzi au wagenzi na walimu au waelekezi, kuwekwa pamoja kwa mbinu hizi mara nyingi huongeza fanaka, matarajio na matokeo ya elimu. Hili huafikiwa kwa kutoa elimu inayooana na taswira zao za asili, mazoea na mitiazamo yao ya ulimwengu. Kwa wanafunzi na walimu wasio wa asili, elimu ya aina hii ina athari ya kuongeza ufahamu wa tamaduni zao za kibinafsi na mazoea ya jumla ya umma na watu wanaowazunguka, hivyo basi kukuza heshima na kuthamini tamaduni za wanajamii hizo.
Katika elimu na mafunzo, kujumuishwa kwa maarifa ya kiasili, tamaduni, maono, mitazamo na dhana katika mitaala, vifaa vya kuelekeza na vitabu vya kozi vina athari kubwa kama ile ya kujumuisha mbinu za asili katika elimu ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Ambayo hunufaisha walimu na wanafunzi katika usambamba wa masomo, kufaulu na matokeo ya masomo hayo. Walimu na wanafunzi wa kisasa wana heshima, hamasa na maridhio kwa jamii na watu wa kienyeji kutokana na elimu husishi wanayopata.[3]
Mfano mkuu unaoonyesha mbinu na maudhui ya asili yanaweza kukuza matokeo yaliyotajwa hapo juu undhihirika katika elimu ya juu nchini Kanada. Kwa sababu ya sheria fulani, dhamira ya kuongeza mafanikio kwa wanafunzi wa elimu asili na kukuza maadili ya jamii ya kitamanduni, kuingizwa kwa mbinu na maudhui ya asili katika elimu huonwa kuwa jukumu na wajibu wa serikali na taasisi za elimu zenye mamlaka.[4]
Mchakato
Mitaala
Mitindo ya kujifunza
Kuna utafiti uliofanyawa kuhusu mitindo ya kusoma katika miongo miwili iliyopita. Dunn na Dunn [6] walilenga kutambua vichangamshi husishi vinavyofanya masomo yavutie na namna ya kutawala mazingira ya shule, baadaye Joseph Renzuli [7] alipendekeza mikikati tofautitofauti ya kufunza. Howard Gardner[8] alitambua talanta ama vipaji vya mtu binafsi katika nadharia zake za akili nyingi. Kwa misingi ya kazi za Jung “Kielezi Aina cha Myers Briggs” na “kitenga tabia cha Keisresy” [9]vililenga kuelewa jinsi nafsi za watu huathiri uhusiano wa mtu binafsi na zinavyoathiri maelewano ya watu katika mazingira ya kujifunza. Kazi za David Kolib na Anthony Gregorc “jinsi ya kusawiri”[10] ” hufuata mfano kama huu lakini uliorahisishwa.Kwa wakati huu, kugawika kwa elimu katika mitindo tofautitofauti hukubalika na wengi. Huenda ikawa kuwa mitindo[11] ya kujifunza ndiyo ya kawaida:[12]
- Kuona: Masomo yenye misingi ya kutazama kwa makini na kuona kile kinachosomwa.
- Kusikiza: Kusoma kwa misingi ya kusikiliza maelezo/habari.
- Masomo husishi: Kusoma kwa misingi ya kutumia mikono na vitendo husishi.
Kujifunza
Walimu wanapaswa kuelewa somo vilivyo ilikuwasilisha umuhimu wake kwa wanafunzi. Shabaha hapa ni kuunda misingi ya ujuzi kamili ambayo wanafunzi wanaweza kutumia kujijenga zaidi kwani wamewekwa wazi kwa matukio mbalimbali ya maisha. Walimu wazuri huweza kutafsiri habari kama hukadiria vizuri, hutumia mazoea na hekima hadi kwa elimu husika ambayo mwanafunzi anaweza kuelewa, kuhifadhi na kupititishia wengine. Utafiti kutoka Marekani unatoa maoni kuwa ubora wa walimu ndio kigezo kinachoathiri mafanikio ya wanafunzi, na kuwa nchi zinazopata alama za juu katika mtihani au majaribio ya kimataifa zimeweka sera chungu nzima zinazohakikisha kuwa walimu wanaoajiri ndio bora. [16]Teknolojia
Teknolojia za habari na mawasiliano (ICT) ni "seti ya vifaa na rasilimali mbalimbali zinazotumiwa kuwasiliana, kuunda, kueneza na kuongoza habari."[17] Teknolojia hizi ni pamoja na kompyuta, mtandao, teknolojia za kusambaza habari (redio na televisheni) na simu. Kuna mvuto unaoongezeka kuhusu namna tarakilishi na mtandao zinavyoweza kuimarisha elimu katika viwango vyote, yaani mseto wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi.[18] Teknolojia za habari na mawasiliano za awali, kama vile redio na televisheni, zimetumiwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa elimu wazi na ile ya mbali, hata hivyo kupiga chapa ndiyo njia nafuu zaidi, inapatikana kwa urahisi, na hivyo basi ni mbinu iliyotawala katika nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.[19]
Matumizi ya tarakilishi na mtandao bado ni changa (ikiwa vinatumika) katika nchi zinazoendelea, na hii ni kwa sababu miundo msingi ni michache na ghali. Kwa kawaida teknolojia kadhaa hutumiwa kwa pamoja bali siyo mbinu moja pekee ya kupokelewa. Kwa mfano, Kothmel Community Radio Internet hutumia matangazo ya redio na kompyuta pamoja na teknolojia ya mtandao, na hivyo hurahisisha kugawa habari na kutoa nafasi za elimu katika kijiji fulani kule Sri Lanka.[20] Chuo kikuu cha Uingereza (UKOU) kilichoanzishwa mwaka wa 1969 kama taasisi ya elimu ya kwanza ulimwenguni kujitolea kutoa elimu ya wazi na ya mbali, bado hutegemea vifaa vilivyopigwa chapa na kuongezea redio, runinga na hivi majuzi programu zilizounganishwa na kompyuta.[21] Vivyo hivyo, Chuo Kikuu cha Indira Gandhi nchini India huweka pamoja matumizi ya chapa, sauti zilizorekodiwa, video, redio, televisheni na teknolojia ya vielezo vya kusikiza mkutano.[22]
Dhana ya “masomo yanayosaidiwa kwa Kompyuta” (CAL) limetumiwa kwa wingi kuelezea teknolojia katika masomo.
Nadharia ya elimu
Uchumi
Katika kiwango cha mtu binafsi, kuna maandishi yenye uhusiano na kazi ya Jacob Mincer, [27] ya jinsi mapato yanahusiana na elimu na rasilimali ya mtu binafsi. Kazi hii imetia motisha idadi kubwa ya utafiti lakini pia inaelekea kuleta mabishano kwa kiasi fulani. Ubishi mkubwa unazunguka jinsi ya kufasiri matokeo ya kusoma.[28]
Wataalam wa uchumi Samwel Bowels na Herbert Ginits walitoa maoni kwamba kulikuwa na ubishi asili katika elimu nchini Marekani kati ya shabaha ya kidemokrasia shirikishi yenye usawa na faida ya mapato ya kikapitolisti yaliyodokeza hali ya kutokuwa na usawa.[29]
Historia
Siku hizi aina fulani ya elimu ni jambo la lazima kwa watu wote katika nchi nyingi. Kwa sababu ya ongozeko la watu na kuenea kwa elimu ya lazima, Shirika La Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepiga hesabu ya kwamba miaka 30 ijayo, watu wengi zaidi watapata elimu rasmi katika historia ya binadamu ulimwenguni.[30]
Falsafa
Saikolojia
Saikolojia ya elimu inaweza kueleweka kwa sehemu kupitia masomo mengine. Saikolojia ya elimu vilevile huarifiwa na saikolojia, ikileta uhusiano baina ya utabibu na bayolojia.[onesha uthibitisho] . Saikolojia ya elimu pia huarifu masafa mapana ya masomo maalum yakiwemo mpango wa mafunzo.[onesha uthibitisho] Teknolojia ya elimu, mtaala uliokuzwa, masomo yaliyopangwa, masomo maalum, sayansi tambuzi na sayansi masomo.[onesha uthibitisho] Katika vyuo vikuu, idara za elimu ya saikolojia vimehifadhiwa katika vitivo vya elimu. Hii ni kwa sababu ya uwezekano wa ukosefu wa uwakilishaji wa maudhui ya saikolojia ya elimu katika utangulizi wa vitabu vya saikolojia.
Sosholojia
Maendeleo ya Kielimu
Katika nchi zinazoendelea idadi na uzito wa shida zilizoko kwa kawaida ni kubwa.[onesha uthibitisho] Watu wa vijijini wakati mwingine huwa hawana habari kuhusu umuhimu wa elimu. Hata hivyo, nchi zingine zina wizara ya elimu na katika masomo mengi kama vile kujifunza lugha za kigeni, kiwango cha elimu kimo juu zaidi kuliko ilivyo katika nchi zilizoendelea. Kwa mfano, ni kawaida kupata wanafunzi katika nchi zinazoendelea wakizungumza lugha nyingi za kigeni kwa usanifu mkubwa ilhali jambo hili ni nadra katika nchi zilizoendelea ambapo idadi kubwa ya watu huzungumza lugha moja.Vilevile kuna shinikizo la kiuchumi kutoka kwa wazazi ambao hupendelea watoto wao wapate pesa kwa muda mfupi kuliko faida za elimu ya muda mrefu.[onesha uthibitisho] Utafiti wa hivi karibuni kuhusu ajira ya watoto na umasikini zimependekeza kuwa familia zilizokumbwa na umasikini zinapofikia kiwango fulani cha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, wazazi huwarejesha watoto wao shuleni.[onesha uthibitisho] Hii imethibitshwa kuwa kweli mara tu kizingiti kinapovukwa. Hata kama uwezekano wa thamani ya kiuchumi ya ajira ya watoto inaongezeka baada yao kurudishwa shuleni.[onesha uthibitisho]
Ukosefu wa vyuo vikuu bora na kiwango cha chini cha kukubalika katika vyuo hivi ni dhahiri katika nchi zilizo na idadi kubwa ya watu.[onesha uthibitisho] Baadhi za nchi zina mitaala mikuu inayoweza kubadilika kwa urahisi, inayofanana na yenye miundo zaidi.
- Kutokana na utandawazi shinikizo kwa wanafunzi katika shughuli za mtaala zimeongezeka
- Kuondolewa kwa asili mia fulani ya wanfunzi kwa ajili ya uboreshaji wa masomo (kwa kawaida hufanywa shuleni baada ya daraja la kumi)
Barani Afrika, shirika la NEPAD limezindua programu ya masomo ya mtandao inayotoa vifaa vya kompyuta na masomo ya mtandao kwa shule zote za msingi na upili kwa kipindi cha miaka kumi. Vikundi vya kibinafsi kama vile The Church Of Jesus Christ Of Latter Days Saints, wanajikakamua kuwapa watu fursa ya kupokea elimu katika nchi zinazoendelea kupitia miradi kama vile Perpetual Educational Fund. Mradi wa maendeleo kimataifa inayofahamika kama nabuur.com, com iliyoanza kutokana na usaidizi wa raisi wa Marekani Bill Clinton, hutumia mtandao kuwezesha ushirikiano wa watu binafsi kuzungumzia maswala ya maendeleo ya jamii.
Umataifishaji
Elimu inaendelea kuwa jambo la kimataifa. Sio vifaa vyake tu vinavyoendelea kuathiriwa na mazingira ya kimataifa yenye ukwasi bali pia mabadiliko ya wanafunzi katika viwango vyote yanayochangia kuendesha jukumu hili muhimu. Kwa mfano kule Uropa, programu ya Socratis Erusmus imechechemua mabadilishano kati ya vyuo vikuu vya Uropa. Vile vile, Shirika la Soros hutoa fursa nyingi kwa wanafunzi kutoka Asia ya kati na Uropa mashariki. Wasomi wengi hudai kwamba ingawa mfumo fulani unaweza kuzingatiwa kuwa bora au mbaya kuliko mwingine, kuzoea aina tofauti ya elimu mara nyingi huonwa kuwa elementi muhimu ya kuzoea masomo ya kimataifa.[33]Dini na Elimu
Tazama makala kuu: Elimu ya kidiniElimu katika dini ya Uislamu ni muhimu kwa wake na waume[onesha uthibitisho], haswa kwa watoto wachanga. Kinyume na dhana ya kawaida[onesha uthibitisho], kutafuta aina zote za maarifa, yawe ya kitaaluma, kidini au ya dunia yanaruhusiwa kwa watu wa umri wowote. Hata hivyo, masomo ya umri mdogo huonwa kuipa akili fursa ya kumakinika bila kuathiriwa na shida na majukumu ya maisha ya utu uzima.[34]
Pia Tazama
- Udanganyifu wa Kielimu
- Elimu ya ngumbaru
- Elimu badala
- Elimu ya kale
- Elimu ya kushirikiana
- Elimu linganishi
- Mtaala
- Masomo ya mtaala
- Curriculum
- Curriculum masomo
- Elimu ya kukua
- Elimu ya mbali
- Elimu ya mtandao
- Elimu ya kielezo
- Mabadiliko Ya elimu
- Elimu ya katuni
- Utafiti wa elimi
- Kielimu utafiti
- Elimu ya teknolojia
- Educational software
- Mbinu mwafaka ya elimu
- Elimu ya biashara
- Elimu ya majaribio
- Elimu ya vipaji
- Faharasa ya maneno yenye uhusiano na elimu
- Elimu ya kuhitimu
- Historia ya elimu
- Kisomo cha nyumbani
- Fundisha
- Teknolojia ya kuelekeza
- Elimu ya lugha
- Kujifunza
- Kusoma 2.0
- Kusoma kwa kufundisha (LdL)
- Jamii inayosoma
- Sayansi ya kusoma
- Elimu ya sheria
- Ujuzi wa maishani
- Elimu maishani
- Orodha ya walimu
- Elimu ya matibabu
- Jamii inayotumia masomo ya mtandao
- Elimu zaidi
- Elimu ya amani
- Kujifunza
- Falsafa ya elimu
- Elimu ya umma
- Elimu ya ziada
- Elimu ya makaazi
- Shule
- Shule ya siku zijazo
- Elimu ya jinsia moja
- Maingiliano
- Sosholojia ya elimu
- Elimu kwa mahitaji maalum
- Uainishaji wa malengo ya elimu
- Mwalimu
- Elimu ya juu
- Kufunza
- Chuo Kikuu
- Elimu kweli na sawa
- Elimu ya kiufundi
- Vitabu vya Wikipidia: Elimu
Marejeo
- UNESCO, elimu kwa wote Ufuatiliaji Report 2008, Net Enrollment Rate katika elimu ya msingi
- Se Merriam et al. Kujifunza kwa watu wazima: A Comprehensive Guide (San Francisco: Jossey-Bass, 2007). Sharan Miriam, Rosemary Caffarella na Lisa Baumgartner wameandika kuwa tunahitaji kuangalia kwa karibu ndani ya mipaka yetu wenyewe, wenyeji wa marekani kwa mfano….. ili kupata mifumo haswa ya fikra na imani zikiwa ndani ya thamani za tamaduni tofauti na mifumo ya epistemilojia ambayo inaweza kutumiwa kupanua uelewa wetu juu ya elimu ya ngumbaru.(uk 218). Merriam wanaendelea kueleza kuwa, azma nyingine ya kupata ufahamu juu ya mifumo mingine ya maarifa, ni faida ambayo maarifa yatakuwa nayo kuathiri utendakazi wetu na wanafunzi walio na mtizamo tofauti isipokuwa ile ya kimagharibi. Antone na Gamlin (2004) kwa mfano wanatoa sababu kuwa programu za kujua kusoma na kuandika za watu asili lazima ziwe zaidi ya kusoma, kuhesabu na kuandika ambako hulenga kufikia ajira kuu' (uk 26). Kwa hakika elimu halisi inahusu kuhifadhi mtazamo maalum na kudumisha tamaduni tofauti na za lazima. Kujua kusoma na kuandika kunahusu kuashiria tena na kutafsiri tena uzoefu uliopita, na kwa wakati huo kuheshimu maadili ya jadi. Uwezo wa kusoma na kuandika kuhusu “kuishi” maadili haya kwa wakati wa sasa. Uwezo huu wa kusoma na wa kuandika unahusu kuwa na maono ya siku za usoni. Asili ya uwezo wa kusoma na kuandika itakuzwa na kupata maelezo katika yote yanayofanywa. Hivyo, programu za asili ya kuweza kusoma na kuandika zinafaa kulenga mtazamo pana unaotambua njia za kipekee ambazo watu asili huwakilisha uzoefu na maarifa yao.(uk 26). Mara kwa mara Merriam na wenzake pia hurejelea mahitaji haya ya “Kutanua uelewa wa elimu ya ngumbaru” kwa kupitia enzi ya utamaduni nyeti nadharia zinazohusiana na mwingiliano wa ndani kati ya masomo na muktadha wa jamii. Kwa kawaida hutazamwa kwa muktadha wa maadili yanayotofautiana, imani, uzoefu, taswira na mazingira yanayowiana na njia za kale na mbinu asili pamoja na fikra za kibinafsi na za kijumla. Kwa mfano katika majadiliano yao, majaribio ya kusoma, waandishi wanatoa maoni kuwa, katika kukubali ujuzi na masomo kutoka kwa uzoefu kama tukio la kitamaduni, taswira … na wasomi wa kisasa huwa muhimu. Kati ya matokeo ya fikra muhimu kuhusu utambuzi kutoka kwa mwegemeo wa utamaduni ni uhakiki ambao umeendelezwa kuhusu nadharia ya elimu ya kale na uzoefu … Muhimu kati ya hizi changanuzi ni changamoto kwa fikra asili kuwa kusoma ni jambo linalofanyika ndani ya mtu binafsi. Kwa hakika, kusoma hujumuisha maingiliano ya wanafunzi na mazingira ya jamii wanamokulia.(uk 180).
- [18] ^Tazama kwa ujumla R.A Malatest na wenzake . Best Practices katika Kuongeza Aboriginal Post-sekondari Enrollment Rates (Kanada: Baraza la Mawaziri wa Elimu, Kanada, 2002) [1][dead link] na Dr Pamela Toulouse, Kusaidia Aboriginal Student Success: Self-Esteem na Identity, A Hai Mafundisho strategin (Presentation mikononi katika Utafiti wa Elimu Ontario 2007 Kongamano) [2]
- Katika mkoa wa Manitoba nchini Kanada kwa mfano, juhudi za pamoja kati ya serikali na taasisi za elimu (vyuo na vyuo vikuu) kumesababisha utekelezaji wa programu 13 za Access. Programu hizi hutilia maanani mbinu na maudhui ya kale katika upokezi wa elimu ya juu; na pia huwapa wanafunzi misaada mbalimbali ya tamaduni nyeti (kama vile wazee na washauri) ili kuzidisha mafanikio katika elimu ya juu. Watetezi wa programu hizi mara nyingi husisitiza kuwa kati ya miaka ya 2001/2002 na 2005/2006 (data iliyopatikana ya hivi karibuni) jumla ya wanafunzi 800 walihitimu kutoka kwa programu hizi na vyeti na asilimia 70.8 ya wanafunzi waliojiandikisha katika miaka hii walikuwa wa usuli wa asili. Takwimu hizi zimetolewa kutoka kur. 141-143 za Manitoba Council on Post-Secondary Education Statistical Compendium for the Academic Years Ending in 2006 [3] halmashauri ya Manitoba kuhusu elimu ya juu. Kulingana na watetezi hawa, kuwekwa pamoja kwa mitindo asili ya elimu ndani ya programu hizo zinazolenga wanafunzi asili, ni kipengele muhimu kinachochangia kukamilika kwa elimu ya juu ya wanafunzi asili waliokisiwa kuwa 566 ambao hawangetarajiwa kuhitimu kiwango hiki cha mafanikio.
- Examples of subjects. Curriculumonline.gov.uk. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Dunn and Dunn. Learningstyles.net. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Biographer of Renzulli. Indiana.edu. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Thomas Armstrong's website detailing Multiple Intelligences
- Keirsey web-site. Keirsey.com. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Type Delineator description. Algonquincollege.com. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Swassing, RH, Barbe, WB, & Milone, MN (1979). The Swassing-Barbe Mfumo Index: Zaner-Bloser mfumo Kit. Columbus, OH: Zaner-Bloser.
- Priscilla Theroux (2004-04-26). Varied Learning Modes. Members.shaw.ca. Iliwekwa mnamo 2009-04-20.
- Barbe, WB, & Swassing, RH, pamoja MN Milone. (1979). Kufundisha kupitia mfumo uwezo: Dhana na mazoea. Columbus, OH: Zaner-Bloser.
- Learning mfumo maelezo kutoka Learning Curve website
- Guy Claxton speaking on What's The Point of School?. dystalk.com. Iliwekwa mnamo 2009-04-23.
- / Jinsi duniani mifumo shule bora hutoka topg
- Blurton, Craig. New Directions of ICT-Use in Education (PDF). Iliwekwa mnamo 2007-02-06.
- IKT katika Elimu
- Potashnik, M. and Capper, J.. Distance Education:Growth and Diversity (PDF). Iliwekwa mnamo 2007-02-06.
- Taghioff, Daniel. Seeds of Consensus—The Potential Role for Information and Communication Technologies in Development.. Jalada kutoka ya awali juu ya 2003-10-12. Iliwekwa mnamo 2003-10-12.
- Open University wa Uingereza Official website
- Indira Gandhi Taifa Open University Official website
- Hanushek, Uchumi Matokeo na Shule ya Quality
- UCLA Economics Qur'ani 183 kutoka Profesa Boustan
- Daron Acemoglu, Simon Johnson, na James A. Robinson, "The kikoloni Chimbuko la Comparative Maendeleo: An Empirical Investigation." American Economic Review 91, no.5 (Desemba 2001) :1369-1401.
- Eric A. Hanushek, na Ludger Woessmann, "Jukumu la cognitive ujuzi katika maendeleo ya kiuchumi." Journal of Economic Literature 46, no.3 (Septemba 2008) :607-608.
- Yakobo Mincer, "Mgawanyo wa kazi kipato: utafiti na kumbukumbu maalumu kwa mtaji mbinu." Journal of Economic Fasihi 8, no.1 (Machi 1970) :1-26.
- Angalia, kwa mfano, Daudi Kadi, "Causal elimu juu ya athari za mapato," katika uchumi Handbook wa kazi, mwisho na Ashenfelter na Daudi Orley Card. Amsterdam: Kaskazini-Holland, 1999:1801-1863; James J. Heckman, Lance J. Lochner, na Petra E. Todd., "Earnings utendaji, viwango vya tiba kurudi na madhara: The Mincer equation na nje," katika Handbook ya ya Uchumi wa Elimu, mwisho na Eric A. Hanushek na Finis Welch. Amsterdam: Kaskazini Holland, 2006:307-458.
- Samuel Bowles na Herbert Gintis, Elimu katika kibepari Marekani: Educational Mageuzi na utata wa Kiuchumi Life (Basic Books, 1976)
- Robinson, K.: Shule Kill Creation. TED Talks, 2006, Monterrey, CA, USA.
- Finn, JD, Gerber, SB, Boyd - Zaharias, J. (2005). Small madarasa katika darasa mapema, mafanikio ya kielimu, na kufuzu kutoka high school. Journal of Educational Psychology, 97, 214-233.
- Schofield, K. (1999). "The Malengo ya Elimu", Queensland State Elimu: 2010, [Juu] URL: www.aspa.asn.au / Papers / eqfinalc.PDF [Accessed 2002, 28 Oktoba]
- Dubois, HFW, Padovano, G., & Stew, G. (2006) Kuboresha muuguzi kimataifa mafunzo: an American-Kiitaliano kesi masomo. Kimataifa Nursing Review, 53 (2): 110-116.
- Inter-Islam> ZZ> Elimu <http://www.inter-islam.org/AZ/E/E.htm#Education>.
Viunganish vya nje
Jua habari zaidi kuhusu Education kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister | |
---|---|
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi | |
Vitabu kutoka Wikitabu | |
Quotations kutoka Wikidondoa | |
Source texts kutoka Wikichanzo | |
Images and media kutoka Commons | |
News stories kutoka Wikihabari | |
Learning resources kutoka Wikichuo |
- Education katika Open Directory Project
- Educational Resources kutoka UCB Libraries GovPubs
- UNESCO Taasisi ya Takwimu: International kulinganishwa mifumo ya takwimu za elimu
- OECD takwimu za elimu
|
No comments:
Post a Comment