AN ONLINE PLATFORM THAT PROVIDES EDUCATIONAL CONTENT ,STUDY MATERIALS, COURSE OUTLINES , PAST PAPERS FOR THE OPEN UNIVERSITY STUDENTS OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND OTHER COLLEGE STUDENTS WORLDWIDE. YOU ARE WELCOME TO SHARE YOUR KNOWLEDGE AND IDEAS. ENYOY THE BLOG.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.THE BLOG IS FREE.
Friday, 28 March 2014
Saturday, 22 March 2014
OSW 226. USHAIRI WA KISWAHILI BY. MWL. JAPHET MASATU
OSW 226. USAHAIRI WA KISWAHILI.
WANA MAMBOLEO NA WANA MAPOKEO
WANATOFAUTIANAJE KATIKA KUELEZA
MAANA YA USHAIRI WA KISWAHILI?
Wataalamu mbalimbali wameeleza maana ya ushairi wa kiswahili, lakini mawazo yao yamefungamana katika sehemu fulani na kuofautiana katika baadhi ya maeneo. wataalamu karibu wote yaani wale wa kimambo leo na kimambo kale kwa pamoja wanaamini kuwa shairi lazima liwe na:
- mpangilio mzuri wa maneno
- lugha inayoeleweka
- lenye kuleta maana kwa hadhira iliyokusudiwa
vile vile wataalamu hawa wa kimamboleo na kimambokale wanatotautiana katika baadhi ya maeneo. maeneno hayo ni pamoja na:
- mpangilio wa urari wa vina na mizani
- mabeti
- kibwagizo au bahari
ZIFUATAZO NI MAANA ZA USHAIRI KULINGANA NA MAWZO YA WANA MAPOKEO
Shaaban
Robert katika Massamba (1983:55) anasema :
“Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa
kama nyimbo, mashairi na tenzi.
Zaidi ya kuwa sanaa
ya vina, una ufasaha wa maneno machache au muhtasari.
Mwauliza wimbo,
shairi na tenzi ni nini? Wimbo ni shairi ndogo, ushairi ni
wimbo mkubwa na
utenzi ni upeo wa ushairi. Mwauliza tena kina na ufasaha
huweza kuwa nini?
Kina ni mlingano wa sauti za herufi. Kwa maneno mengine
huitwa mizani ya
sauti na ufasaha ni uzuri wa lugha. Mawazo na maoni na
fikra za ndani
zinapoelezwa kwa muhtasari wa shairi huvuta moyo kwa namna
ya ajabu”.
Naye Abdilatifu Abdalla katika Massamba
(1983:57) anasema:
“Utungo ufaao kupewa jina la ushairi si utungo
wowote bali ni utungo ambao katika kila
ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya
chenziye, wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani. Na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato
maalum na yenye lugha nyoofu, tamu na laini. Lugha ambayo ina uzito wa fikra,
tamu kwa mdomo wa kusema, tumbuizi kwa masikio ya kusikia na yenye kuathiri
moyo uliokusudiwa na kama ilivyokusudiwa”.
Mayoka (1986:3) anasema:
“Ushairi ni mtungo wa kisanaa ulio na
mpangilio maalum wa lugha ya mkato ambayo ndani yake ina vina, urari wa mizani
na muwala maalum ambavyo kwa pamoja huwa na fani na maudhui yahusuyo hisi
fulani au tukio juu ya maisha ya mtu au
watu wa mazingira na wakati maalum”.
WANA MAMBO LEO
Wangari
na Mwai (1988:5) wanaonesha kuwa washairi wa kisasa wanaeleza kwamba fasihi
hubadilika katika umbo na maudhui na kwa hiyo ushairi wa Kiswahili sharti
uruhusu mabadiliko yanayotokea katika ushairi huru.
Mulokozi na Kahigi (1979:25) wanasema:
“Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa
mpangilio maalum wa maneno fasaha yenye muwala, kwa lugha ya mkato, picha au
sitiari katika usemi, maandishi, au mahadhi ya wimbo ili kueleza wazo au
mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu maisha au mazingira ya
binadamu kwa njia inayogusa moyo”
Friday, 21 March 2014
OSW 227. RIWAYA YA KISWAHILI ---- BY. MWL. JAPHET MASATU.
OSW 227. RIWAYA YA KISWAHILI.
Riwaya
ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu zaidi kuliko
hadithi fupi. Urefu wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi
umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, inaenea muda mrefu, na mada zake
ni nzito na pana kiasi. Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, riwaya za mwandishi Euphrase Kezilahabi.
Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K.W. Wamitila inataja aina nyingi tofauti za riwaya, k.m. riwaya changamano, riwaya sahili, riwaya kiambo, riwaya ya kibarua na nyingi nyingine.
Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K.W. Wamitila inataja aina nyingi tofauti za riwaya, k.m. riwaya changamano, riwaya sahili, riwaya kiambo, riwaya ya kibarua na nyingi nyingine.
Uandishi wa riwaya
== Uhariri wa riwaya == mizimu ya watu wa kaleMarejeo
Wamitila, Kyallo Wadi (2003), Kamusi ya Fasihi - Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Publications. ISBN 9966-882-79-6
Jamii:
- Fasihiumbani
sarufi
fasihi
isimu jamii
insha
msamiati
jukwaa
RIWAYA YA KISWAHILI.
RIWAYA Utanzu wa Fasihi Fasihi Andishi Kiingereza Novel Mifano Kiu, Siku Njema, Mwisho wa Kosa Angalia
Prev Tamthilia Next Hadithi Fupi Content
Aina za Riwaya
Kunazo aina kadhaa za Riwaya katika Fasihi Andishi:- Riwaya sahili - visa vyake husimuliwa moja kwa moja na huwa rahisi kueleweka
- Riwaya changamano - hii ni riwaya ambayo huhitaji kusomwa kwa makini ili kueleweka. Aghalabu huwa na maudhui mengi na wahusika wengi ambao wanachangia katika tatizo kuu katika riwaya hiyo. Hujengwa kwa taharuki ili kuwavutia hadhira kutazamia jinsi tatizo kuu litakavyotatuliwa. Hutumia mbinu za taharuki na visengere nyuma/mbele.
- Riwaya ya kibarua - hutumia muundo wa barua kuwasilisha ujumbe wake.
- Riwaya kiambo - huhusisha maswala ya kawaida katika jamii
Mifano ya Riwaya
- Utengano
- Siku Njema
- Mwisho wa Kosa
- Kiu
- FASIHI SIMULIZI
- Hadithi / Ngano
- Nyimbo
- Maigizo
- Tungo Fupi
- FASIHI ANDISHI
- Hadithi Fupi
- Riwaya
- Tamthilia
- Aina za Wahusika
Friday, 14 March 2014
OSW 221. SARUFI YA KISWAHILI SINTAKSI ---- CHUO KIKUU HURIA TANZANIA.
OSW 221. SARUFI YA KISWAHILI
SINTAKSIA/SINTAKSI --CHUO KIKUU HURIA TANZANIA.
Sintaksi (au sarufi miundo/muundo) ni tawi la isimu au taaluma ya sarufi inayoshughulikia namna ambavyo vikundi vya maneno na sentensi mbalimbali zinajengwa katika lugha.
Hasa hushughulikia kanuni zinazotawala mfumo wa vipashio vya lugha.
Sarufi muundo hushughulikia kanuni zinazotawala mpangilio wa maneno
katika lugha husika ili kujenga (kuunda tungo yenye maana). Kipashio ni
kipande cha neno au kikundi cha maneno yanayotoa taarifa fulani katika
lugha ya Kiswahili. Kuna vipashio vitano - navyo ni: Mofimu --> Neno
--> --> Kirai --> Kishazi --> Sentensi. Katika namna ya
kutaja au kutumia vipashio, ngazi ya mofimu ni ndogo kuliko neno. Neno
ni ndogo kuliko Kirai. Kirai ni kidogo kuliko Kishazi. Kishazi ni kidogo
kuliko Sentensi. Hivyo basi mpangilio wake halisi huanza kwa ukubwa na
kuja udogo.
Mfano, ukubwa kwenda udogo:
5. Sentensi
4. Kishazi
3. Kirai
2. Neno
1. Mofimu
Taaluma nyingine za sarufi ni pamoja na fonolojia, mofolojia au semantiki.
Mfano, ukubwa kwenda udogo:
5. Sentensi
4. Kishazi
3. Kirai
2. Neno
1. Mofimu
Taaluma nyingine za sarufi ni pamoja na fonolojia, mofolojia au semantiki.
Marejeo
- TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Tazama pia
- Lango la lugha
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sintaksi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.SINTAKSIA
MIKABALA YA TAALUMA YA SARUFI.(a) Sarufi ubongo(b) Sarufi kama kaida za kiisimu.(c) Sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha.UTANGULIZI WETU UTAZINGATIA MAMBO YAFUATAYO· Maana ya sarufi.· Mkabala wa kimapokeo.· Mkabala wa kisasa.· Ufafanuzi wa sarufi ubongo· Ufafanuzi wa sarufi kama kaida za kiisimu· Ufafanuzi wa sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha.· Tofauti zilizopo katika mikabala hii.Katika mjadala huu, kwanza kabisa tutaanza kwa kuangalia dhana muhimu ambazo zimejitokeza katika mada yetu, ambazo ni sarufi, mkabala wa kimapokeo pamoja na mkabala wa kisasa. Kisha tutangalia kwa kujadili kiini cha mada, ambapo tutaangalia jinsi sarufi ubongo, sarufi kama kaida za kiisimu na sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha na inaangukia katika mkabala upi na inatofautiana vipi.Tukianza na maana ya sarufi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali kama vile:-Kihore na wenzake (2005) wakimnukuu Gaynor (1968:88), wanaeleza kuwa sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake.Vile vile Mdee (1999) anafasili sarufi kama mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi nyingi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha.Pia Massamba na wenzake (1999:31) katika mtazamo wa pili wa kufasili dhana ya sarufi wanaeleza kuwa sarufi ni kanuni sheria au taratibu za uchambuzi zinazotawala lugha.Hivyo basi wanasarufi hawa wanaonekana kukubaliana kwamba sarufi ni kanuni, sheria na taratibu zinazotawala lugha. Lakini kwa kiasi kikubwa tunakubaliana na fasili iliyotolewa na Mdee kutokana na kwamba ameweza kutufafanulia vizuri kanuni hizo na taratibu za lugha ndizo zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi nyingi, sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha.Kwa mfano:- sentensi za kiswahili zina muundo waN + V + T + EMtoto mzuri anacheza uwanjani.
N V T E
Baada ya kuangalia dhana ya sarufi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali sasa tunaweza kuangalia mikabala mikuu miwili ya sarufi ambayo ni:-i. Mkabala wa kimapokeoii. Mkabala wa kisasa.Kwa kuanza na mkabala wa kimapokeo kwa mujibu Khamisi na Kiango (2002), wanaeleza kuwa hii ni sarufi ya kale, wataalamu wanaohusishwa na mkabala huu walijitokeza kuanzia karne ya 5 kabla ya kristo na katika karne ya 18 na karne ya 19 baada ya kristo, wataalamu hao ni kama vile Plato, Aristotle, Panin, Protagoras ambao walijihusisha na lugha kwa kutaka kujua asili yake ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa asili ya maumbo hususani walitaka kujua kama lugha ni tukio la maumbile au tukio la unasibu.Pia Massamba na wenzake (wameshatajwa) wanaeleza kwamba sarufi mapokeo zilikuwa ni sarufi elekezi ambazo zilisisitiza kanuni na nini cha kusema na wajua lugha. Watu wasiojua kanuni za lugha wanapaswa kujifunza kutoka kwa wanaojua sarufi ya lugha. Wanaendelea kusema kuwa, wanaojua lugha hupaswa kutunga kanuni za sarufi.Vile vile Habwe na Karanja (2004:124), wanadai kuwa mitazamo hii ya wanasarufi hawa wa kimapokeo iliathiri mbinu na njia za kuangalia lugha kwani sarufi mapokeo ilijikita katika lugha za kiulaya kama vile kiyunani na kilatini.Sifa mbalimbali za lugha hizi ambazo ziliaminiwa kuwa bora, zilichunguza kilatini na kiyunani zilielezwa kuwa ni lugha duni na kutwezwa na kudhalilishwaSarufi mapokeo ilielekeza watu jinsi ya kutumia lugha, uelekezi huo hata hivyo ulijikita kwenye sheria za lugha ya kilatini kwa mfano sentensi haikupaswa kuishia na kihusishi wala kuanza na kiunganishi.Udhaifu mkubwa wa sarufi mapokeo ni kwamba, taratibu za uchanganuzi wa lugha hazikuzingatia lugha ya kuzungumza kama ilivyo leo. Wanasarufi mapokeo walienzi na kuchunguza lugha ya maandishi. Hivyo basi ni dhahiri kwamba mkabala huu unaangukia katika mitazamo ya kifalsafa.Hivyo basi ni wazi kuwa katika sarufi hii ya mapokeo tunakutana na mikabala miwili inayoangukia katika mkabala huu ambayo ni sarufi ubongo na sarufi kama kaida za kiisimu.Mkabala wa pili, ni mkabala wa kisasa, unaoongozwa na wanasosiolojia ambao unahusisha sarufi mbalimbali kama vile :-i. Sarufi msongeii. Sarufi miundo viraiiii. Sarufi geuza maumbo zalishiiv. Sarufi husianoKatika mkabala huu ndipo tunapata mkabala wa sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha.Hivyo basi baada ya kujadili mikabala mikuu miwili ambayo ni mkabala wa kimapokeo na mkabala wa kisasa, zifuatazo ni sifa muhimu za sarufi ubongo, sarufi kama kaida za kiisimu na sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha ambazo kwazo tutaona jinsi kila moja inavyotofautiana na nyingine.Kwa kuanza na sarufi ubongo, kwa mujibu wa Nordquist (2012), anaeleza kuwa sarufi ubongo ni sarufi endelevu ambayo inamwezesha binadamu kuzalisha lugha ambayo inaweza kueleweka kwa wenginePia Sharpe (2006), anaeleza kuwa sarufi hii hufananishwa na umilisi, anaendelea kueleza kuwa sarufi hii humwezesha mtu kuweza kusikia na kutambua kama sentensi hiyo ni sahihi au si sahihi.Chomsky (1957), anaeleza kuwa kila binadamu amezaliwa na uwezo wa kuzalisha tungo mbalimbali zisizo na ukomo ambazo humpatia uwezo au uzoefu wa sarufi ya lugha. Pia anafafanua kwamba kila binadamu huzaliwa na kifaa katika ubongo wake ambacho kinamwezesha kuamili lugha ya aina yoyote, amekiita kifaa cha uamiliaji lugha (KIULU). Kwa mfano mtoto mdogo mwenye umri chini ya miaka saba anaweza kuamili lugha yoyote na mahali popote.Mgullu (1999), anaeleza kuwa sarufi ubongo huchunguza jinsi binadamu anavyojifunza lugha kwa mfano hatua mbalimbali ambazo hupitia wakati anajifunza lugha yake ya kwanza.Kwa hiyo tunakubaliana na fasili zote zilizotolewa na wataalamu hapo juu kutokana na kwamba sarufi ubongo, hii ni sarufi ambayo inachunguza jinsi binadamu anavyoweza kuamili lugha na kujifunza lugha pia kuweza kuzalisha sentensi mbalimbali ambazo anaweza kuzitumia katika mawasiliano.Vile vile wataalamu wa mkabala huu hueleza kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya akili, kufikiri na lugha bila shaka uhusiano huu ni ule wa taathira ya lugha yaani dhana inayoeleza kuwa kwa kawaida kila lugha huathiri watumiaji wake kwa kiasi kikubwa.Vile vile wataalamu wa mkabala huu wanaeleza jinsi watu wanavyojifunza lugha ya pili au lugha ya tatu.Kwa kifupi mkabala huu hujihusisha na mambo kadha kama vile:-(i) Kumwezesha binadamu kuweza kuzalisha au kutunga sentensi mbalimbali.(ii) Sarufi ubongo huusika na uamiliaji wa lugha na ujifunzaji wa lugha.(iii) Sarufi hii huwakilisha maarifa ya mzungumzaji wa lugha (umilisi alionao mzungumzaji).Mkabala mwingine wa sarufi ambao unaangukia katika mkabala wa sarufi mapokeo ni sarufi kama kaida za kiisimu.Kwa mujibu wa Encyclopedia (1970), wanaeleza kuwa sarufi kaida ni mpangilio unaoonyesha au kueleza kanuni za kisarufi katika lugha ambazo hushughulika na kanuni za uundaji wa maneno, maumbo ya maneno, miundo ya maneno, miundo ya sentensi, vile vile inahusisha taarifa maalumu kuhusu fonetiki na fonolojia (taaluma inayohusika na utamkaji sahihi unaokubalika)Pia kwa mujibu wa Babylon Dictionary (1997), wanaeleza kuwa sarufi kaida ni mfumo wa kisarufi ambao unafafanua kipi sahihi na kipi si sahihi katika lugha, pindi mzungumzaji anapozungumza, amezungumza sahihi au si sahihi.Kwa hiyo tunaweza kueleza kuwa sarufi kaida hujishughulisha sana na:-i. Kuelekeza namna ya matumizi sahihi ya lugha.ii. Wataalamu wa lugha ndio wanaounda kanuni na miongozo ya lugha ambayo inatakiwa kufuatwa na wale wasiojua lugha.Kwa mfano:- kanuni mojawapo ya miundo ya sentensi za Kiswahili huwa na muundo wa kiima na kiarifu.Vile vile sentensi nyingi za Kiswahili huwa na muundo wa kirai nomino na kirai kitenzi.Hivyo basi katika mkabala huu wa sarufi watu wasiojua lugha wanapaswa kufuata kanuni na taratibu zilizoundwa na wanaojua lugha kwa mfano wanasarufi.Pia mkabala mwingine wa sarufi ambao unaangukia katika mkabala wa kisasa ni sarufi kama utafiti na uchambuzi wa miundo inayoonekana katika lugha.Kwa mujibu wa Besha (2007), anaeleza kuwa huu ni mkabala unaohusika hasa na uchambuzi wa muundo wa lugha, sauti za lugha, muundo wa sentensi na hata maana za tungo za lugha.Pia mgullu (1999), anaeleza kuwa lengo la mkabala huu ni kufafanua vipengele vyote vya lugha fulani kama vilivyo hivi sasa au vilivyokuwa wakati fulani.Hivyo basi Besha na Mgullu wanakubaliana kuwa huu ni mkabala unaofafanua namna au jinsi watu wanavyozungumza lugha na sio kuwaelekeza waizungumze vipi lugha yao.Hivyo basi kwa ujumla mkabala huu unajihusisha na mamba yafuatayo:-i. Hautilii mkazo mabadiliko yaliyotokea katika lugha hata kama mabasiliko hayo yapo.ii. Mkabala huu hauamuru watu waseme vipi na vipi wasiseme.Kutokana na sifa mbalimbali zilizojitokeza katika mikabala hii, tumeweza kubaini tofauti zilizopo baina ya mikabala hii mitatu ambazo ni kama zifuatazo:-Sarufi ubongo, sarufi kama kaida za kiisimu zinajitokeza katika mkabala wa kimapokeo wakati sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha inajitokeza katika mkabala wa kisasa.Vilevile sarufi ubongo humwezesha binadamu kuweza kuzalisha miundo mbalimbali ya tungo wakati sarufi kama kaida za kiisimu haijihusishi kabisa na masuala ya ubongo bali yenyewe hujihusisha na mazoea ya kawaida ya watumiaji wa lugha ambapo kunakuwa na makosa ambayo huwafanya wataalamu kuunda kanuni za lugha ambazo zinatakiwa kufuatwa na wasiojua lugha hii inatofautiana na sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyoonekana kwenye lugha kwa kuwa haihusiani na masuala ya ubongo wala kaida, bali yenyewe hujihusisha na utafiti na ufafanuzi wa miundo ya lugha kama inavyotumika na wazungumzaji wa lugha na haiwaelekezi jinsi ya kuzungumza.Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kwamba pamoja na tofauti hizo zilizojitokeza katika mikabala hiyo mitatu, mikabala hii inaonekana kufanana kwani yote inajihusisha na lugha ya binadamu, pia mikabala hii imechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya taaluma ya isimu na ndio imekuwa darajia kwa wataalamu mbalimbali katika kufanya tafiti zao kwa mfano baada ya kushindwa kwa sarufi ubongo na sarufi kama kaida za kiisimu ndipo kukazaliwa kwa sarufi kama tafiti na uchambuzi wa miundo inavyooneka kwenye lugha.MAREJEOBabylon Dictionary. (1997). Translation and Information Platform. Babylon Ltd.Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa lugha na Isimu. Macmillan Aidan Ltd. Dar es Salaam.Chomsky, N. (1957). Syntactic Structures. Mouton The Hague.Khamis, A.M na John G.K (2002). Uchanganuzi wa sarufi ya Kiswahili. TUKI. Dar es salaam.Habwe, J na Peter K (2007). Msingi ya sarufi ya Kiswahili.Phoenix Publishers. Nairobi.Kihore, Y.M na wenzake. (2008). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA):Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es Salaam.
Massamba, D.P.B. na wenzake. (2009). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na Vyuo. TUKI.Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers Ltd. Nairobi.Sharpe J. P (2006). Barron’s How to prepare for the TOEFL IBT. Barron’s Educational Series.The Great Soviet Encyclopedia. (1970). (3rd ). The Gale group. Moscow.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sintaksi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Subscribe to:
Posts (Atom)