Wednesday 9 April 2014

ISIMU JAMII NI NINI ? BY. MWL JAPHET MASATU.

ISIMU    JAMII   NI    NINI ?    BY.    MWL.    JAPHET      MASATU.

  

 Kuna wataalmu mbalimbali ambao wameeleza maana ya isimu ,kwa mfano BESHA anasema kuwa  Taaluma ambayo inachunguza na kuweka wazi kanuni ambazo ndizo msingi wa kila  lugha.    Nayo kamusi ya lugha (TUKI) (taaasisi ya uchukuzi ya lugha) ,inaeleza kuwa ismu ni sayans ya lugha.isimu nitaaluma am bayo inahakiki lugha kisayansi.Ni sayansi ya kimatashi , miundo maumbo na matamshi ya
                                       
                   USAYANSI WA ISIMU               
Wanaisimu walio chunguza lugha waliyumbishwa na mitazamo na mielekeo yao ,ndiposa wakaona haja yakuichunguza kisayansi.
           SIFA ZA UCHAMBUZIWA LUGHA KISA 
 (1)uwazi
Hii inawataka wanaisimu kuweka hoja zao wazi bila tashwishwishwi yoyote ile.Hii ina maana ya kwamba mada ya uchunguzi yafaa kuelezwa kwa undani k abisa.yote ambayo wanaisimu watayasema kuhusu mada yawe kwa uwazi na kwa njia ya kueleweka kwa urahisi.kwa mfano mawanda aliyo yatumia katika kazi yake yawe na uwazi na ukamilifu ambao unafaa kuzingatiwa katika uwekaji wa maneno utengaji wa hoja na hata uchunguzi wa data
(2)upangilifu na utaratibu maalum
Hoja zote zinapaswa kupanga vzuri katika taaluma zote za kisayansi hufuatwa, kwa utaratibu  maalum mambo yote hufuatwa hatua kwa hatua. Wanaisimu hufuata utaratibu katika kuchambua kazi yake ifaavyo .mwanaisimu hatakiwi kufanya kazi yake kiholela holela.


(3)uchechefu
hapa ni pale wanaismu wanapofaulu kueleza tofauti zote zilizomo katika kongoo linalochunguzwa a hatimaye katika lugha hiyo yote.

(4)wanaisimu kuweza kuifafanua kazi yao jinsi inavyotakikana
hii ni hatua ambapo mwanaisimu anapofanikiwakuifafanua kazi yake kwa undani kabisa, katika viwango vyote.viwango hivi ni kama vile vya kifonolojia ,mfumo wa sauti na kimofolojia.


(5)mwana isimu anafaa kuichunguza kaz yake kwa kina kabisa
mwanaiimu anapofanikiwa kueleza yale yote ambayo ametafiti kwa kina ,bil kuacha au kupuuza kitu chochote anachochunguza.

          
                                        
           
MALENGO YA ISIMU

ISIMU INA MALENGO MENGI ZAIDI KATIKA JAMII. MALENGO NI KAMA VILE
(1)Isimu huweza kuchunguza lugha nyingi katika jamii
(2)isimu huweza kumulika yale yote yanayojitokeza katika lugha
(3)isimu huweza kuchambua lugha tofauti ,kwa undani kabisa

(4)isimu huweza kuchanganua na kufafanua lugha kwa undani



                                 MATAWI YA ISIMU
Kuna matawi mengi sana ya isimu ambayo husaidia katika uchambuzi wa lugha. matawi haya ni kama yafuatayo

(1)Isimu  jamii.
 hili ni tawi la isimu ambalo ,hueleza masuala yote muhimu yanayodhihirisha uhusiano uliopo baina ya lugha  na jamii husika .maswala muhimu ambayo huchunguzwa ni kama vile ,
                                  sera za lugha
                                   lahaja
                                     rejista
                                     usanifishaji wa lugha
(2)isimu tumizi
tawi hili hushughulikia zaidi matumizi ya nadharia ya kiisimu katika kueleza mambo mbalimbali ya kiisimu.
(3)isimu historia
tawi hili huchunguza mabadiliko yanayotokea katika lugha fulani kati kipindi cha muda fulani wa histoia ya lugha inayohusika.mabadiliko haya yanaweza kuwa ya kimofolojia fonolojia sintaksiana hata semantiki.mabadiliko haya yanaweza kuwa ya kidaikronia au kisinkroni.
kidaikronia, uchunguzi hufanywa katika nyakati mbalimbali. kisinkronia , kkufanya uchunguzi wa lugha kwa wakati maalumu
(4)isimu fafanuzi
hili ni tawi la isimu ambalo huchunguza vipengele vyote vya lugha jinsi ilivyo au ilivyokuwa hapo awali.
(5)ismu linganishi

lengo la tawi hili la isimu ni kuchunguza lugha mbalimbali na kuzilinganisha na kuzilinganua.wanaisimu huchunguza lugha katika viwango vyote vikiwemo vya kimofolojia kifonolojia na kisemantiki
(6)ISIMU KIAFRIKA.
Tawi hili la isimu huchunguza lugha zinazozungumziwa barani afrika .Wanaisimu huzichunguza lugha hizi  na kuzifafanua kwa undani.kisha huzigawa katika makundi ya kinasaba.
(6)ISIMU TIBA
tawi hili la isimu hushughulikia urekebishaji wa dosari za lugha zinazowapata watu kwa kutumia utaalam wa juu wa kiisimu.hii ni isimu ambayo hutatua mata tizo ya kuzungumza.
(7)ISIMU NAFSIA
huchuguza jinsi binadamu anavyojifunza lugha.wanaisimu wengi wataeleza hatua nyingi ambazo mtoto hupitia wakati ambapo anajifunza lugha yake ya kwanza.pia hutatua matatzo yanayoikumba lugha na  jinsi ya kutatua matatizo hayo.
  

No comments:

Post a Comment