Friday 25 April 2014

KF 102 : UTANGULIZI WA FASIHI SIMULIZI NA ANDISHI

KF  102: UTANGULIZI   WA   FASIHI   SIMULIZI  NA   ANDISHI.

Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu maalum kwa ajili ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu cha msingi ya utamaduni, na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.
Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi—hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.
Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Hata hivyo, mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.

Viungo vya Nje

No comments:

Post a Comment